Tanzania ni nchi yetu pendwa inayojulikana duniani kote kama kisiwa cha amani katika Afrika Mashariki. Tangu tupate uhuru mwaka 1961, nchi yetu imesimama imara kama mwamba wa utulivu na umoja. Wakati nchi jirani kama Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Burundi zikikabiliwa na migogoro ya kisiasa na kijeshi, na Kenya ikipitia maandamano yanayoleta hasara kubwa, Tanzania inaendelea kuwa na amani ya kweli. Hii ni matunda ya uongozi thabiti wa serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mheshimiwa Rais Dr Samia Suluhu Hassan na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinachotawala kwa hekima na kujali maisha ya wananchi.

Amani yetu ni hazina kubwa ambayo inavutia wawekezaji na kuleta maendeleo. Serikali imetenga fedha nyingi kwa elimu, afya, barabara na miradi ya vijana. Hakuna vita wala migogoro mikubwa ya kikabila hapa. Badala yake, raia wanaishi pamoja kwa upendo na hekima. Hii inafanya Tanzania kuwa mahali salama pa kuishi na kufanya biashara.

Wengine wanajaribu kuwahamasisha vijana kufanya maandamano na ghasia. Hii si njia sahihi kwani inaharibu amani, inatisha wawekezaji na kuwanyima fursa za maendeleo. Serikali inasisitiza mazungumzo na ushirikiano badala ya vurugu. Kumbuka maneno ya Mwalimu Julius Nyerere: amani ni muhimu kuliko yote.

Vijana ndio nguvu ya taifa. Fursa ziko nyumbani katika kilimo, madini, utalii na teknolojia. Serikali inawapa mikopo, mafunzo na msaada wa kuanzisha biashara. Usikimbilie nje, anza hapa na uijenge Tanzania pamoja. Tuilinde amani yetu kwa kushirikiana na serikali na kuepuka chocheo cha migogoro. Amani ndiyo ufunguo wa maendeleo yetu.

Mungu ibariki Tanzania. Amani na umoja!